Monday, August 19, 2013

Re: YAH: OMBI LA SAFARIYA KWENDA CANADA.




From: Amisi Joshua <amisi_joshua2011@yahoo.com>
To: "tomaszbentkowski1_zachodniwbk@live.com" <tomaszbentkowski1_zachodniwbk@live.com>
Cc: "eddie@mail-elbajawelry.com" <eddie@mail-elbajawelry.com>
Sent: Sunday, August 18, 2013 8:28 PM
Subject: YAH: OMBI LA SAFARIYA KWENDA CANADA.

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa UN husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Sisi ni watoto wa Mzee Joel Kabiluba Kihota wa asili ya Congo ambao tulipewa majibu ya barua zetu za maombi ya kupewa Hati za ukimbizi za tarehe 13/ 12/ 2012 na kujibiwa tarehe 20 Aprili 2013 Kumb. Na. Ke 27/ 378/ 05 C/ 102, 103, 104, 105, 106 na 107 kwa watoto wote sita zilizo sahiniwa na Afisa A. KWEKA kwa niaba ya Katibu Mkuu wake zilizokuwa zinasema: tuliwakilisha maombi yetu ya kupewa hadhi ya ukimbizi baada ya jitihada za kusaidiwa kuungana na wazazi wetu wanaoishi Canada kama wakimbi kushindikana kwa kukosa ushahidi kuwa nasi ni wakimbizi hapa nchini kwa mujibu wa sheria ya wakimbizi wa mwaka 1998.
Wametumwa kwako ili wapewe fursa ya kuhojiwa juu ya madai yao ya ukimbizi na kikao cha NEC yaani National Eligibility Committee.
Afisa huyo alijisahau kwa namna moja au nyingine kwa hilo, wakati Mzee wetu yaani Baba yetu alionyesha Paspoti yake ya Canada katika Ofisi hiyo ya Uhamiaji kama raia wa canada na sio mkimbizi tena.
Mnamo tarehe 30/ 05/ 2013, baada ya kuhojiwa na NEC hiyo pale Kigoma NMC, NEC katika uamuzi wao ilikubali kutupa Hati za ukimbizi sawasawa na maombi yetu .
Mnamo tarehe 17/ 06/ 2013, tulirudi tena hapa Dar es salam baada ya kuruhusiwa na NEC  kufanya hivyo na tarehe 10/ 07/ 2013, tulienda kwenye ofisi ya IOM Dar es salaam , Tanzania. Tulifanya mahojiano na Afisa mmoja wa kiume katika ofisi hiyo, alitujibu kuwa IOM haihusiki na swala binafsi au la watu wengi., ila inahusika na swala linaloletwa na makundi mawili au matatu kama vile: 
1. UNHCR,   2. WAFADHILI,   3. SERIKALI.
Afisa huyo ambaye hakutaja jina lake alisisitiza kuwa njia zote hizo ni muhimu kwa ajili ya msaada kwetu, ila shirika la IOM ndilo ambalo linawasafirisha wakimbizi kutoka katika nchi ya pili na kwenda nchi ya tatu, na fedha hizo hulipwa kidogokidogo hadi pale mtakapo maliza deni hilo lote.
Idara ya Uhamiaji bado wanaendelea kutushurutisha mara nyingine tena kurudi kambini kwa kuwa wanasema kuwa Serikali haipendi kumweona mkimbizi yeyote nchini hapo, wote wataendelea kuishi kambini na waliyowengi wao watarudishwa Congo kwa nguvu.
Sisi watoto wa Mzee Joel Kabiluba Kihota hatuwezi kwenda tena kambini na pia hatuwezi kurudishwa Congo kwa sababu zifuatazo:
1. Wote tumezaliwa nchini Tanzania.
2. Baba yetu alikuwa mwanasiasa pamoja na Laurent Desire Kabila, baadaye wakatengana na kuwa maadui baada ya Laurent Desire Kabila kuingia na raia wakigeni kutoka Tanzania hadi nchini Congo, na sisi watoto pia tukawa maadui wake kwa kuungana au kukubaliana na mawazo ya Baba yetu kisiasa.
3. Kisiasa hatuwezi kuendelea kuishi hapa Tanzania na hata pia ndani ya Congo kwa sababu katika madai yetu tunasema nchi yetu hiyo inatawaliwa na wageni na hata Rais Hypolite Christophe kwa jina bandia Jeseph Kabila anayeitawala Congo ni mtutsi wa Rwanda kwa baba na mama aliyesomea nchini hapa na kuwa mwanajeshi wa Tanzania.
Hivyo Mheshimiwa Katibu Mkuu tunaomba msaada wako haraka ili tupate kuepukana na maangamizi haya ya kisaikolojia, kielimu, kisiasa pamoja na kiuchumi.
Nimatumaini yetu tutapata majibu mazuri kwako. Tunatanguliza shukrani zetu kwako kwa kulipokea ombi  letu na Mungu akubariki sana.

Kwa niaba ya familia :
Ebuela Ibrahim Mboko Kabiluba.
Amisi Lungwe  Joshua  Kabiluba.


No comments:

Post a Comment